Kituo hicho kimetoa taarifa hiyo mapema Jumatatu na kusema kwamba idadi ya vifo duniani kutokana na ugonjwa huo imefikia milioni tano laki nne na ishirini na tano, miezi minne tu baada ya kufikia milioni nne.
Kwa Pamoja Marekani, Jumuiya ya ulaya, Uingereza na Brazil, nchi zote zenye kipato cha kati au cha juu zinajumuisha karibu nusu idadi ya watu wote duniani waliokufa.
Marekani peke yake imerekodi vifo 746,000, ambayo ndiyo idadi kubwa zaidi kuliko ya mataifa mengine.
Idadi ya vifo iliyorekodiwa na chuo kikuu cha John Hopking ni karibu sawa na idadi ya Los Angeles na San fransisco zikiunganishwa pamoja.
Hata hivyo taarifa zinasema bara la Africa linaendelea kubaki kuwa chini katika utoaji wa chanjo.
Kuna asilimia 5 tu ya watu bilioni 1.3 waliopata chanjo kamili katika bara hilo.