Wakenya watatu wanaotuhumiwa kwa uchochezi wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007 na 2008 nchini Kenya alhamisi wamefika katika mahakama ya uhalifu ya kimataifa ya uholanzi ambapo septemba mosi ICC imesema itaamua kama wana kesi ya kujibu au hapana.
Waziri wa zamani wa elimu William Ruto , waziri wa viwanda Henry Kosgey na mtangazaji wa Radio Joshua Arap Sang walikuwa katika mahakama – The Hague, kujibu mashtaka dhidi ya uhalifu wa binadamu.
(Video ya ICC PIDS)
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Luis Moreno-Ocampo aliwatuhumu watuhumiwa wote sita kwa kupanga ghasia zilizosababisha vifo vya watu 1, 300 na kukosesha makazi wengine laki tatu.
Ghasia hizo zilizuka baada ya matokeo ya uchaguzi wa marudio mwaka 2007 kutangazwa. wote rais Mwai Kibaki na na kiongozi wa upinzani Raila Odinga walidai kuwa wameshinda .