Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:36

ICC inaamrisha mashtaka dhidi ya Bemba


Kiongozi wa chama cha MLC Congo Jean Pierre Bemba akipiga kura yake Kinshasa, wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Congo Jumapili Julai 30, 2006.
Kiongozi wa chama cha MLC Congo Jean Pierre Bemba akipiga kura yake Kinshasa, wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Congo Jumapili Julai 30, 2006.

Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa huko The Hague, imesema kwamba kiongozi wa zamani wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba ni lazima ajibu mashtaka mahakamani kwa tuhuma za uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

ICC ilikata siku ya Jumanne rufaa iliyowasilishwa na mawakili wa Bemba walotoa hoja kua, mahakama hiyo ya Kimataifa haikua na mamlaka ya kisheria kwa sababu inapatikana huko Uholanzi na wala si Afrika.

Waendesha mashtaka wa kimataifa wanasema, vikosi vya Bemba vilitenda maovu na mateso ikiwa ni pamoja na ubakaji na mauwaji huko Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2002 wakati vilikua vinamsaidia rais Ange-Felix Patasse kukabiliana na jaribio la mapinduzi.

Mawakili wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wamewatuhumu mawakili wa Bemba kwa kujaribu kuzuia kesi kuendelea.

Bemba alikua makamu rais wa DRC mwaka 2003 kama sehemu ya makubaliano ya amani ya nchi hiyo, na baadae kushindwa katika uchaguzi wa rais na kushtakiwa kwa uhaini.

XS
SM
MD
LG