Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 11:15

ICC yajadili afya ya Gbagbo


Rais wa zamani wa IvoryCoast Laurent Gbagbo, kushoto, na rais aliye madrakani Alassane Ouatarra, kuia.

Mahakama ya uhalifu ya kimataifa inafanya kikao cha siku mbili cha kusikiliza juu ya afya ya rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, ambaye anakabiliwa na kesi The Hague iliyoahirishwa hadi Januari.

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, na kiongozi wa wanamgambo Charles Ble Goude, wote walitakiwa kusikilizwa kesi zao katika mahakama ya ICC hio jana, Badala yake, mahakama hiyo, inafanya kikao cha faragha, pale wataalam wanapotowa ushahidi kuhusu hali ya afya ya Bw. Gbagbo.

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:02:36 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Msemaji wa ICC Fadi El Abdallah anaeleza kuwa, mawakili wa Bw. Gbagbo wameomba mahakimu wa ICC kuruhusu watetezi na wahusika wengine kuuliza maswali wataalam, kwa hivyo hicho ndicho kitakacho fanyika katika siku mbili za kesi hio.

Wote Gbagbo na Ble Goude wanakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadam. Mashtaka hayo yanahusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 na 2011 huko Ivory Coast. Takriban watu elfu 3 waliuwawa baada ya Gbagbo kukataa kuachia madaraka kwa mshindi wa uchaguzi huo, Alassane Ouatarra.

Hapo siku za nyuma, mawakili wa Bw. Gbagbo walihoji uwezo wa kiafya wa bw Gbagbo kuweza kushiriki katika kesi hiyo, lakini msemaji wa ICC Fadi El Abdullah anasema uwezekano wa kufuta kesi, ambayo sasa imepangwa kuanza hapo Januari 28 mwaka ujao , anasema suala hilo halijajadiliwa.

Kesi ya Bw Gbagbo itakuwa ya kwanza kwa rais wa zamani katika taifa kufikishwa mbele ya mkondo wa sheria kwenye mahakama ya ICC. Mahakama hiyo pia ilijaribu kufungulia mashtaka mkewe Gbagbo bi Simone Gbagbo, lakini haikufanikiwa .

Param Preet Singh, mshauri mkuu wa pragramu ya sheria kutoka shirika la Human Rights Watch anasema, ukweli kwamba Gbagbo yuko huko the Hague, unaeleza mengi juu ya uwezo wa mahakama ya ICC.

Bi. Singh anasema, wakati kesi ya Gbagbo ni mapinduzi kwa mahakama, anasema kuna hisia huko Ivory Coast kwamba mahakama ya ICC inapendelea upande mmoja. Anasema, kulikuwa na wafuasi watiifu kwa rais Ouatarra ambao pia walitenda uhalifu, lakini hawakusakwa na mahakama ya ICC.

Bw Ouattarra amabye alichaguliwa tena mwezi ulopita kama rais, ameahidi kuwafikisha wahusika wa ghasia za baada ya ucahguzi mbele ya sheria.

Msemaji wa ICC Fadi El Abduallah anasema waendesha mashtaka wa mahakama hiyo wanaendelea kufanya uchunguzi juu ya tuhuma dhidi ya pande zote. Mahakam hiyo itachukuwa hatua nasema Bw Abduallah mara tu itakapopata ushahidi wa kutosha.XS
SM
MD
LG