Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 14:15

Hungary yatangaza hali ya dharura


Mwanamke na watoto wake akitumia njia ya Reli kuelekea kwenye mpaka wa Serbia na Hungary

Pengo lililopo baina ya Hungary katika uzio unaopakana na Serbia kwa wiki kadhaa limetumika na wahamiaji kama sehemu kubwa ya kuingia kinyume cha sheria.

Hungary imetangaza hali ya dharura katika majimbo mawili kama sehemu ya ukandamizaji kwa wahamiaji wanaojaribu kuingia bara la ulaya.

Maafisa wa hungary wamesema leo kwamba pia wamefunga mipaka miwili kutokana na kile wanachosema ilikuwa vigumu kudhibiti eneo la Serbia.

Msemaji wa serikali ya Hungary Zoltan Kovacs amesema kutokana na hali iliyosababishwa na uhamaji mkubwa , serikali yake imetangaza hali ya dharura , mzozo ambao utawezesha polisi na maafisa wengine wa usalama walioko katika eneo kufuata itifaki.

Amesema wahamiaji wanaojaribu kuingia nchini kinyume cha sheria watarejeshwa.

wahamiaji wakisubiri kuvuka mpaka wa Serbia kuingia Hungary
wahamiaji wakisubiri kuvuka mpaka wa Serbia kuingia Hungary

Pengo lililopo baina ya Hungary katika uzio unaopakana na Serbia kwa wiki kadhaa limetumika na wahamiaji kama sehemu kubwa ya kuingia kinyume cha sheria.

Jumanne mamia ya wahamiaji waliingia na kuvuka vizuizi vilivyopo wakidai waruhusiwe kukatisha mpaka huku wakipaza sauti , “fungua mpaka, fungua mpaka”, wakati polisi wakiwa wamesimama upande mwingine. Polisi imewakamata watu 60 chini ya sheria mpya ambayo inaweza kupelekea watu waliovuka mpaka kinyume cha sheria kufungwa karibu miaka mitatu jela.

XS
SM
MD
LG