Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 18:27
VOA Direct Packages

Human Rights Watch lashinikiza Russia kutoa taarifa za alipo mfungwa wa kisiasa


Andrey Pivovarov ambaye ni mfungwa wa kisiasa nchini Russia.
Andrey Pivovarov ambaye ni mfungwa wa kisiasa nchini Russia.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema Jumamosi kwamba hatua ya Russia ya kukataa  kutoa taarifa kuhusu alipo mfungwa mmoja wa kisiasa imezua wasi wasi kuwa huenda amepotezwa kwa lazima.

Familia ya Andrey Pivovarov pamoja na wakili wake wamesema hawajaweza kuwasiliana naye tangu Januari 18, pale alipoandika barua akiwafahamisha kuwa anahamishwa kutoka jela ya St Petersburg hadi kwenye jela nyingine isiyojulikana.

Kupitia taarifa, HRW limesema kwamba Russia inahitaji kumuondolea kifungo hicho na kumuachilia mara moja, na kwa sasa iruhusu familia yake pamoja na wakili wamuone.

Julai mwaka jana, Pivovarov alihukumiwa kifungo cha miaka minne kwa kuongoza vugu vugu la kisiasa la Open Russia Civic Movement kinyume cha sheria. Tangu Desemba amekuwa akihamishwa kutoka jela moja hadi nyingine, ila familia yake wala wakili hawakufahamishwa.

XS
SM
MD
LG