Jaji Thokozile Masipa wa Afrika kusini atatoa uamuzi Jumatano juu ya ombi la mwendesha mashtaka la kukata rufaa kupinga hukumu yake dhidi ya mwanariadha Oscar Pistorius.
Jaji Masipa alisikiliza hoja Jumanne katika chumba hicho hicho cha Mahakama iliyoendesha kesi mjini Pretoria.
Hapo ni mahala ambapo mwezi Oktoba, Jaji Masipa, alitangaza hukumu ya kuuwa bila kukusudia na kifungo cha miaka mitano kwa Oscar Pistorius.
Hukumu hiyo kwa Pistorius ni kwasababu ya kumfyatulia risasi mpenzi wake wa kike, Reeva Steenkamp.
Pistorius hakuwepo mahakamani Jumanne wakati mwendesha mashtaka Gerrie Nel alipozungumzia upinzani wake akisema hukumu haikotolewa kisahihi.