Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:32

Huduma ya kutuma fedha Somalia mashakani


Mwanamume akipokea fedha zilizotumwa kutoka ng'ambo katika kituo cha Dahabshiil mjini Mogadishu.
Mwanamume akipokea fedha zilizotumwa kutoka ng'ambo katika kituo cha Dahabshiil mjini Mogadishu.
Benki ya Barclays ya Uingereza ilitangaza Jumatano kuwa siku ya mwisho ya kufanya biashara ya kuhamisha fedha kwenda Somalia na kutishia chanzo kikuu cha fedha kwa Wasomali wengi. Hata hivyo iliamua kuongeza muda huo kwa makampuni mengi lakini wakaazi wa Somalia wana Khofu juu ya hali ya baadaye endapo huduma hiyo ya kifedha itafutwa.

Biashara ya kuhamisha fedha nchini Somalia ni kuu. Umoja wa Mataifa unakisia kuwa Somalia hupokea dola bilioni 1.2 kila mwaka kutoka nje ya nchi, fedha ambazo zinasaidia ujenzi mpya wa taifa hilo baada ya kulemazwa na miongo mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Lakini mwezi jana, benki ya Barclays ya Uingereza ilisema inafuta kabisa huduma hiyo ya kuhamisha fedha kupitia makampuni kadha ya Somalia kutokana na khofu kwamba pengine fedha hizo zitatumika kufadhilia shughuli za kigaidi. Benki hiyo ilitangaza Julai 10 kuwa siku ya mwisho ya kutoa huduma hiyo, lakini baadaye ikaongeza muda ili makampuni hayo yatafute benki nyingine za kutoa huduma hiyo.
Mwakilishi wa mojawapo ya kampuni kubwa Dahabshiili iliyopo Mogadishu anasema biashara iliendelea kama kawaida Jumatano. Lakini raia wana khofu kubwa kuhusu kufungwa kwa huduma hiyo.

Ikitangaza uamuzi huo mwezi jana, benki ya Barclays ilisema baadhi ya makampuni ya biashara hizo za kifedha hayana njia za kukagua kubaini ikiwa fedha hizo zinatumiwa kufadhili ugaidi na uhalifu mwingine.

Benki za Marekani zilisimamisha huduma za kuhamishia fedha kwenda Somalia kutokana na khofu kwamba huenda zikakiuka sheria za Marekani dhidi ya kufadhili magaidi, zikileng kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye ushirika na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida.
XS
SM
MD
LG