Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 02:42

HRW yatoa ripoti ya ndoa za utotoni Tanzania


Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch lenye makao makuu yake New York, Marekani

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch-HRW limezindua ripoti inayoelezea namna ndoa za utotoni zinavyoathiri malezi na haki ya kupata elimu kwa baadhi ya watoto wa kike nchini Tanzania ambapo utafiti unaonyesha kuwa kati ya wanawake 10, wanne huolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18.

Mwandishi wa utafiti huo juu ya ndoa za utotoni Brenda Akia kutoka Huma Rights Watch alisema kwamba katiba inayopendekezwa nchini Tanzania haijatoa umri unaotakiwa kuoa au kuolewa.

Hata hivyo Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 imeweka umri wa miaka 18 kwa wanaume kuoa na miaka 15 kwa wanawake kuolewa kwa ridhaa ya mzazi au mlezi vile vile imeruhusu mtoto wa kike au wa kiume wa miaka 14 kuoa au kuolewa kwa ruhusa ya mahakama.

Wakati huo huo Dr. Hellen Kijo Bisimba ni mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu yeye alisema kunahitajika utashi wa kisiasa katika kubadili sheria zinazokandamiza mtoto wa kike nchini tanzania

Ripoti hiyo ya Human Rights Watch ilihusisha utafiti kwa kuwahoji takribani wasichana na wanawake 135 katika wilaya 12 nchini Tanzania pamoja na viongozi wa kiserikali, wanaharakati na watu waliopo kwenye mashirika ya kimataifa nchini Tanzania.

XS
SM
MD
LG