Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 15:50

Hospitali ya Muhimbili yasitisha huduma


Hospitali ya Muhimbili yasitisha huduma
Hospitali ya Muhimbili yasitisha huduma

Mgomo wa madaktari Tanzania wasitisha huduma za afya

Huduma za matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Muhimbili nchini Tanzania
zimesimama kwa muda usiojulikana kutokana na mgomo wa madaktari unaoendelea, mgomo ambao sasa umepata sura mpya kufuatia madaktari bingwa nao kuingia kwenye mgomo huo. Madaktari hao bingwa wameanzisha mgomo wakiinishikiza serikali kuyapa uzito malalamiko yao ambayo ni pamoja kuboreshwa kwa mazingira ya kazi. Mgomo huu unazorotesha kwa kiwango kikubwa sekta ya afya, hasa wakati wanapojitokeza madaktari bingwa ambao hapo awali walijiweka kando na mgomo ulionzishwa na madakatri walioko kwenye mafunzo ya vitendo.Tayari hospitali ya kitaifa ya Muhimbili imetangaza kulemewa na mzigo na imeamua kusitisha kwa muda shughuli za utoaji matibabu. Kwingineko ikiwemo hospitali ya Ocean Road ambayo mahususi kwa ajili ya matatizo ya kansa, hali siyo ya kuridhisha. Wagonjwa wanaendelea kutaabika huku wengine wakilalamika kutokana kwa kukosa huduma. Baadhi ya ndugu na jamaa waliowaleta wagonjwa wao kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya Muhimbili, sasa wanaanza kufunganya virago kurejea makwao lakini bila kupewa huduma yoyote ya matibabu.Wakati huo, huo maafisa wa Kituo cha sheria na haki za binadamu wamekutana na waandishi wa habari na kutoa tamko la kulaani kadhia hiyo. Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Bi Hellen Kijo Bisimba,ameinyoshea kidole serkali. Kwa hivi Kamati ya Bunge inayohusika na masuala ya Jamii imekamilisha kuendesha vikao vyenye shabaha ya kutanzua mkwamo huu.

XS
SM
MD
LG