Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:03
VOA Direct Packages

Homa ya ndege aina ya H5N1 yaripotiwa Paris, Ufaransa


Picha ya ndege walioripotiwa kubeba homa ya
H5N1 nchini Cambodia, katika picha ya maktaba.
Picha ya ndege walioripotiwa kubeba homa ya H5N1 nchini Cambodia, katika picha ya maktaba.

Shirika la kimataifa la afya ya wanyama WOAH, limesema Jumanne kwamba Ufaransa imeripoti mlipuko wa homa ya ndege aina ya H5N1 miongoni mwa mbweha kaskazini mashariki mwa Paris, wakati kuenea kwa virusi hivyo miongoni mwa wanyama wakiwemo wanadamu kukizua wasiwasi.

Shirika hilo limeongeza kusema kwamba mbweha mmoja miongoni mwa watatu waliopatikana wakiwa wamekufa kwenye mbuga ya wanyama ya Meaux, alifanyiwa majaribio kwenye maabara na kudhibitishwa kuwa na homa hiyo.

Shirika la afya duniani ,WHO, mwezi uliopita lilieleza wasiwasi wake kutokana na kuongezeka kwa maambukizi hayo miongoni mwa ndege na wanyama, wakati likitadhmini hatari zake ulimwenguni, zikiwemo kesi za maambukizi ya binadamu hivi karibuni nchini Cambodia.

Homa ya Avian maarufu bird flu imekuwa ikienea kote ulimwenguni katika mwaka mmoja uliopita, na kuuwa zaidi ya ndege milioni 200. Homa hiyo inasemekana kuambukiza paka mmoja nchini Ufaransa Decemba iliyopita.

XS
SM
MD
LG