Wanaharakati wa kisiasa wanaelezea khofu ya kurudi kwa ghasia zinazohusiana na uchaguzi nchini Kenya licha ya uthabiti ulioshuhudiwa kwa miaka minne sasa. Wanaharakati wa makundi ya kiraia wanaamini kuwa mageuzi ya kisiasa ya karibuni hayatoshi kuzuia ghasia nyingine kutokea.
Makundi ya haki za kiraia nchini Kenya yalikusanyika mjini Nairobi kuzungumzia njia za kuhamasisha utawala bora na uchaguzi wa amani wakati uchaguzi mkuu nchini humo ukikaribia mwezi Machi 2013.
Mhadhiri Kimani Njogu, mkuu wa Twaweza Communication aliiambia Sauti ya Amerika-VOA- kuwa mageuzi ya kisiasa yaliyofanyika nchini humo ikiwemo kuipitisha katiba mpya, hayajasitisha ghasia. “Katiba yenyewe ni hati nzuri sana, lakini kuwa yenyewe haitoshelezi. Ninafikiri kuna kazi nyingi ambazo zinahitajika kufanywa ili kufuata imani ya katiba, utumiaji na utekelezaji wake”.
Mapigano ya kikabila ya karibuni katika eneo la Tana Delta yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 100, ikiwemo maafisa polisi, yameongeza khofu miongoni mwa wa-Kenya na yamefanya wajiulize maswali juu ya uwezo wa serikali yao kuingilia kati na kusitisha mapigano ya kikabila.
Njogu anasema kanuni mpya katika katiba ambazo zinatoa madaraka zaidi kwa magavana zinaongeza mvutano katika uchaguzi ujao na kusababisha uwezekano wa ghasia za kiwango cha juu kuliko zile za mwaka 2007.
Kenya ilishuhudia wimbi la mashambulizi na ghasia za kikabila kufuatia upigaji kura wa nafasi ya kiti cha rais katika uchaguzi uliopita uliokuwa na utata. Kiasi cha watu 1,300 waliuwawa na zaidi ya 300,000 waliondolewa kutoka kwenye nyumba zao.
Serikali ya mseto ya Kenya inauhakika kwamba mageuzi yanayotekelezwa yatazuia ghasia kutokea wakati wa uchaguzi wa safari hii, lakini baadhi ya Wakenya wanakhisi kuwepo na dalili za ghasia.