Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 20:31

Hillary Clinton atangaza kugombea urais Marekani


Hillary Rodham Clinton akihutubia mkutano New York City March 10, 2015.
Hillary Rodham Clinton akihutubia mkutano New York City March 10, 2015.

Hillary Clinton, mke wa rais wa zamani Bill Clinton, ametangaza kuwaanagombania urais wa Marekani mwaka 2016.

Kulingana na John Podesta, mshauri mwandamizi wa Bi Clinton waziri wa mambo ya nje katika awamu ya kwanza ya Rais Barack Obama, alitangaza nia yake kwa kutuma email Jumapili kwa wafadhili na watu waliomuunga mkono katika kampeni yake ya kwanza ya urais mwaka 2008.

Baadaye Clinton alitangaza rasmi ugombea wake katika chama cha Democratic kwa njia ya video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii. Vyanzo vya habari vinasema anapanga kusafiri kwenda katika majimbo muhimu inayopiga kura za mwanzo, ikiwa ni pamoja na Iowa and New Hampshire.

Endapo hatimaye atachaguliwa kuwa rais, Clinton atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Marekani.

Hillary Clinton aanza kampeni za kugombania urais 2016
please wait

No media source currently available

0:00 0:06:41 0:00

Hii ni mara ya pili kwa Hillary Clinton kuwania urais wa Marekani baada ya kushindwa na Barack Obama mwaka 2008 kupata ugombea wa chama cha Democratic.

Akizungumza kutoka Panama Jumamosi, Rais Obama alisema Clinton atakuwa "rais mzuri sana."

"Alikuwa mshindani imara mwaka 2008. Aliniunga mkono sana katika kampeni yangu ya uchaguzi mkuu. Alikuwa hodari sana kama waziri wangu wa mambo ya nje. Ni rafiki yangu. Nadhani atakuwa rais mzuri sana," alisema Rais Obama.

Clinton, mwenye umri wa miaka 67, anatazamiwa kushinda uteuzi wa mgombea wa chama cha Democratic.

Kabla hajatangaza, Warepublican walijaribu kumhusisha Clinton na Obama ambaye bila shaka watamlenga sana katika sera zao wakati wa kampeni.

XS
SM
MD
LG