Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:58

Clinton na Trump wapeana vijembe katika hafla ya Catholic Charity


Mgombea wa chama cha demokratic Hillary Clinton akitoa hotuba yake huku mpinzani wake Donald Trump akitabasamu wakati wa hafkla ya mlo wa jioni kwa ajili ya kuchangia watoto ulioandaliwa na kanisa katoliki mjini New York. Oct. 20, 2016.
Mgombea wa chama cha demokratic Hillary Clinton akitoa hotuba yake huku mpinzani wake Donald Trump akitabasamu wakati wa hafkla ya mlo wa jioni kwa ajili ya kuchangia watoto ulioandaliwa na kanisa katoliki mjini New York. Oct. 20, 2016.

Wagombea urais wa Marekani, Hillary Clinton na Donald Trump hawakujizuia kutoleana maneno katika hafla ya chakula cha jioni ya kila mwaka kwa ajili ya kutoa misaada mjini New York, wakati wa kutoa hotuba zao ambazo ni utamaduni wa kutoa vichekesho kwa kila mmoja anayegombea urais, nchini Marekani lakini walijikuta wakishambuliana.

Katika mlo huo wa jioni wa kumbu kumbu ya Alfred E.Smith ambao huandaliwa na taasisi ya hisani ya Catholic Charity wagombea hao wawili walikaa meza moja na kutoa maneno ya kuchekesha katika hotuba zao siku moja baada ya mdahalo uliokuwa na ushindani mkali na maneno makali dhidi ya kila mmoja kuwahi kutokea katika historia ya Marekani.

Trump ambaye alianza kuzungumza katika usiku huo alichukua nafasi hiyo kufanya utani juu ya jambo ambalo limezungumzwa sana katika uchaguzi wa mwaka huu kuhusu tabia na mwenendo wake.

Clinton nae kwa upande wake alianza hotuba yake kwa kutoa utani juu ya hali ya afya yake ya hivi karibuni na fedha anazolipwa.

XS
SM
MD
LG