Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 14:24

Hillary aweka historia kuwa mwanamke wa kwanza kuwania urais Marekani


Watu wakiwa katika ufunguzi wa daraja la mto Nile nchini Uganda
Watu wakiwa katika ufunguzi wa daraja la mto Nile nchini Uganda

Vyombo vya habari vya Marekani vilibashiri Clinton atakuwa na wajumbe wa kutosha kuwa chaguo la Democratic katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba. Pia vyombo hivyo vya habari vya Marekani vilisema Clinton tayari ana wajumbe 2,383 wanaomuunga mkono ambao aliwahitaji ili kupata uteuzi wa chama.

Hii inajumuisha wajumbe wakuu ambao wapo huru kumuunga mkono mgombea yeyote lakini tayari wameahidi kumuunga mkono Clinton.

Mgombea mtarajiwa wa urais kwa chama cha Republican, Donald Trump amemshambulia vikali anayeonekana mpinzani wake kutoka chama cha Democratic, Hillary Clinton siku ya Jumanne akimshutumu kwa kuuza fursa kwa wizara ya mambo ya nje ya Marekani wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje.

Mgombea urais wa Republican, Donald Trump
Mgombea urais wa Republican, Donald Trump

Trump alitoa maneno makali alisema Clinton na mume wake, Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton wamegeuza siasa kujinufaisha binafsi.

Trump alisema lengo lake ni kuwajumuisha watu pamoja na aliahidi kutorudi nyuma katika mapambano au kuwaangusha wafuasi wake. Trump alizungumza katika usiku wakati ambao Hillary Clinton aliweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kupata uteuzi usio rasmi wa chama ili kuwania urais. Baada ya uchaguzi wa awali katika majimbo sita uliofanyika siku ya Jumanne.

XS
SM
MD
LG