Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 07, 2024 Local time: 18:35

Hezbollah yashambulia Israel


Kundi la wanamgambo wa Lebanon,  Hezbollah, limerusha makombora ya kukabiliana na vifaru na mabomu dhidi ya msafara wa jeshi la Israel katika eneo lenye ghasia la mpakani na kumuua raia wa Israel, kundi hilo na jeshi la Israel limesema Ijumaa.

Hezbollah imesema kuwa wapiganaji wake waliuvizia msafara huo muda mfupi kabla ya saa sita usiku Alhamisi, na kuharibu magari mawili.

Jeshi la Israel limesema shambulizi hilo la kuvizia limemjeruhi raia wa Israel aliyekuwa mfanyakazi wa miundombinu, na baadaye alifariki kutokana na majeraha yake.

Mapigano kidogo katika mpaka wa Israel na Lebanon yametishia kuzusha ghasia wakati Israel ikiwalenga wanamgambo wa Hezbollah katika miezi ya hivi karibuni.

Mapigano yamesababisha vifo vya raia 10 na wanajeshi 12 kwa Israel, huku Lebanon, zaidi ya watu 350 wameuawa wakiwemo raia 50 na wanamgambo 271 wa Hezbollah.

Forum

XS
SM
MD
LG