Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 14:38

Obama aidhinisha majeshi ya Marekani kusaidia zaidi Afghanistan


Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha hatua zaidi kwa majeshi ya Marekani huko Afghanistan kusaidia majeshi ya nchi hiyo kupambana na Taliban.

Mpango huo mpya ambao unafuatiliwa na mdahalo wa miezi kadhaa utaruhusu ongezeko la mashambulizi ya anga dhidi ya Taliban inapobidi na kuwapa zaidi uwezo Marekani jinsi ya kushirikiana na majeshi ya Afghanistan.

Uamuzi huo utabadili upya ushirikiano wa Marekani na majeshi ya Afghanistan ikiwa ni zaidi ya mwaka sasa tangu majeshi ya kimataifa kumaliza operesheni zao na kuacha majeshi ya Afghanistan kupambana na Taliban.

XS
SM
MD
LG