Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 23:54
VOA Direct Packages

Matokeo ya uchaguzi yawastaajabisha wengi Marekani


Kura zinaendele kuhisabiwa kufuatia uchaguzi wa katikati ya muhula katika jimbo la Arizona.

Udhibiti wa bunge la Marekani bado haujaamuliwa mpaka Jana usiku huku zoezi la kuhesabu kura likiendelea katika ushindani wa viti kadhaa vya Seneti na Wawakilishi kote nchini.

Huku baadhi ya Warepublican waliotarajiwa kushinda wakijikuta wakishindwa katika ushindani huo, Wademocrat bado huenda wakashikilia udhibiti kwa wingi mdogo.

Mwandishi wa VOA. Katherine Gypson anaripoti nini kitafuata ikiwa hakuna chama kitapata wingi wa viti.

Rais wa Marekani Joe Bide bado hafahamu kama atafanya kazi na bunge ambalo linadhibitiwa na wademocrat katika miaka miwili ijayo, lakini tayari amejitangazia ushindi.

Rais Biden alisema: “Wakati vyombo vya habari na wachambuzi wanabashiri kuhusu wmbi kubwa jekundu hilo halikutokea.”

Rais Biden
Rais Biden

Kihsitoria, marais wa Marekani wameshuhudia wakipoteza viti vingi kwenye vyama vyao wakati wa uchaguzi wa katikati ya muhula.

Lakini wademocrat wameshinda katika majimbo yaliyokuwa na ushindani mkali sana kama Virginia nje kidogo ya Washington DC na kuwazuia Warepublican kupata wingi mkubwa katika Bunge.

Mwakilishi wa Republican Kevin McCarthy bado huenda akawa spika ajaye wa Baraza la Wawakilishi.

McCarthy alisema: Warepublican watafanya kazi na mtu yeyote ambaye yuko tayari kujiunga na sisi kutekeleza huu mwelekeo mpya ambao wamarekani wanautaka.”

Lakini wachambuzi wanasema ajenda yake haitakuwa tu kushughulika na wabunge waliodhinishwa na Trump. Inaelezewa MCarthy atakuwa na wakati mgumu sana kuweza kuhimili mshikamano, kwasababu hivi sasa huenda wakawa na wingi mdogo kwahiyo kutahitajika mbinu kwanjia yoyote ile ili kuweza kuleta muungano.

Pia kulikuwa na matokeo yasiyotarajia kwa ushindani wa karibu sana kote nchi nzima ikiwemo ushindi katika jimbo la kaskazini mashariki la Pennyslvania, John Fetterman alimshinda mgombea wa Republican Dr. Mehmet Oz ili kuleta uwezekano kwa Wademocrat kuwa na wingi katika baraza la Senate.

John Fetterman
John Fetterman

Fetterman alisema: “Kulinda haki ya mwanamke kuchagua, kuongea kima cha chini cha mshahara, huduma za afya ni haki za msingi za binadamu.”

Wachambuzi wanasema vipaumbele hivyo vitakuwa vigumu kuvipitisha kama wademocrat watakuwa na kura ya maamuzi ya Makamu Rais Kamala Harris.

Kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili wapiga kura wa Georgia huenda wakawa na maamuzi juu ya udhibiti wa baraza la senate katika duru ya pili ya upigaji kura kati ya seneta Mdemocrat Raphael Warnock na mgombea Mrepublican Herschel Walker. Baadhi ya wapiga kura wa Georgia wanasema ni muhimu kutotoa mamlaka kwa chama chochote.

Na pia wanafahamu kuhusu gharama ya kuhamisha mamlaka kutoka chama kimoja kwenda kingine.

Hatima yau wiano wamadraka huenda isijulikane mpaka December 6, wakati wapiga kura watakapochagua kati ya Warnock na Walker.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG