Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 01:01

Hali yazidi kuwa mbaya Syria


Dazeni ya walinda usalama wa Syria, na waasi wameuwawa katika shambulio katika jengo la ujasusi mjini Aleppo, kundi la uangalizi linataarifu.

Kundi la “Syrian Observatory for Human Rights,” linasema shambulizi lilianza baada ya bomu kulipuka katika njia ya chini kwa chini karibu na jengo la upelelezi la jeshi la anga.

Wanajeshi wa serikali 20 na wanamgambo 14 waliuwawa na shambulizi ambalo limefanywa na kundi lenye uhusiano na Al-Qaida la Nusra Front na vikundi vingine vya waislamu wenye msimamo mkali.

Tarifa iliyosambazwa na wafuasi wa Nusra Front, kwenye mtandao wa Twitte, kundi hilo limesema Mujaheedeen, wameangamiza jengo hilo na walikuwa wanapigana katika maeneo mengine.

Alepo, imegawanyika baina ya vikosi vya serikali na makundi yanayopigana kumuondoa rais Bashar Al-Assad, katika mzozo wa miaka mine unaokadiriwa kusababisha vifo vya 200,000.

XS
SM
MD
LG