Hilo ni pamoja na kuongezeka kwa taharuki za kikabila. OCHA limesema kwamba mapigano mapya kati ya jeshi la Sudan na kundi la kijeshi la Rapid Support Forces, RPF, kwenye pande zote za Darfur, yameuwa darzeni ya watu pamoja na kuharibu mali zao.
Ripoti zimeongeza kusema kwamba takriban watu 17 wameuwawa huku 35 wakijeruhiwa katika wiki moja iliyopita huko Nyala, kusini mwa Darfur, wakati wengine 17,500 wakilazimika kutoroka makwao.
Mapigano ya kijeshi pamoja na ya kikabila pia yameripotiwa Kaskazini na Kati mwa Drafur, ambapo watu zaidi wameuwawa, huku wengine wakifurushwa makwao. Msemaji wa OCHA Jens Laerke ameongeza kuwa watu wa Darfur wameteseka kwa muda mrefu na hasa wanawake kwenye mapigano ya miaka ya nyuma na yanayoendelea sasa hivi.
Forum