Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:57

Waafrika milioni 200 wanalala na njaa kila siku


Baadhi ya watu wakiandaa chakula kinachotokana na zao la muhogo barani Afrika.
Baadhi ya watu wakiandaa chakula kinachotokana na zao la muhogo barani Afrika.
Wataalamu wa kiafrika, wakulima na wadau wamekamilisha siku mbili za majadiliano kuhusu njia za kulisha idadi ya watu wanaoongezeka katika bara hilo na kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa mujibu wa program ya mazingira ya Umoja wa Mataifa-UNEP, waafrika milioni 200 wanalala njaa. Hiyo ni asilimia 23 ya watu. Takwimu za mwaka huu kuhusu usalama wa chakula zinaonesha nchi nane kati ya 10 zenye usalama mbaya sana wa chakula zipo barani Afrika.

Mratibu wa Umoja wa Mataifa katika mabadiliko ya hali ya hewa kwa Afrika, Richard Munang anasema kuna haja ya kuongeza uzalishaji chakula ili kulisha watu bila kuwepo shinikizo juu ya mfumo wa ekolojia katika bara hilo.

Mpatanishi wa kundi moja la Afrika katika mkutano, Emanuel Dlamini, anaeleza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yataendelea kuwepo, lakini serikali za kiafrika na wakulima wanatakiwa kuangalia njia za kukubali hilo.

Nchi nyingi za barani Afrika zinategemea mvua ili kuandaa mashamba yao na kuanza kupanda mazao. Kwa miaka kadhaa iliyopita nchi kadhaa zimekumbwa na ukame na kufanya watu wake kutegemea msaada wa chakula.

Wakulima wa kiafrika wanalalamika kwamba mvua za siku hizi hazitabiriki na ongezeko la joto kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha mazingira ya kuwepo magonjwa ya mazao ambayo yanaathiri uzalishaji.

Mwakilishi wa Nestle Africa, Hans Johr anasema wakulima wanahitaji msaada kutoka makampuni yanayotengeneza vyakula na taasisi zisizo za kiserikali ili kukabiliana na changamoto.

Waandaaji na washiriki wa mkutano huo wanatoa wito wa juhudi za pamoja kutoka jumuiya ya kimataifa, serikali na wakulima kufanya kazi pamoja kuongeza uzalishaji wa chakula na pia kuingilia usalama wa chakula na kilimo endelevu katika sera za bara na za kimataifa.
XS
SM
MD
LG