Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 08:40

Hali ya chakula Afrika


Mboga na matunda
Mboga na matunda
Ni nchi saba tu kati ya nchi 53 za Umoja wa Afrika ambazo ziliahidi kutenga takriban asili mia 10 ya bajeti yake ya kitaifa kuwekeza katika kilimo na kufikia malengo yao.

Mashirika ya kutoa misaa yanasema uwekezaji katika kilimo ndiyo chanzo muhimu cha kuvunja ukosefu wa usalama wa chakula katika eneo la Afrika Magharibi.

Na huku maadhimisho ya miaka kumi ya makubaliano hayo yakisherehekewa wiki hii mashirika fadhili yanataka nchi za Umoja wa Afrika kutimiza ahadi waliotoa katika mkutano wa Maputo.

Mnamo mwaka wa 2003, viongozi wa nchi 53 za Afrika walikubaliana kutenga takriban asili mia 10 ya bajeti zao za kitaifa kuwekeza katika sekta ya kilimo na mifugo ifikapo Julai 2008.

Lakini miaka 10 baadaye ni Burkina Faso, Niger, Guinea, Mali , Malawi na Ethiopia zilizofikia lengo hilo. Nchi nyingi kama vile Nigeria, Guinea Bissau na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo zimetenga asili mia 3 tu ya bajeti yake kwa uwekezaji wa kilimo.Hii ni licha ya kwamba wakulima wenye mashamba madogo wanawakilisha asili mia 80 ya raia wao.
XS
SM
MD
LG