Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:10

Hali mbaya yakumba wakimbizi Kenya


wakimbizi wakiwa katika kambi ya Ifo huko Dadaab, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.
wakimbizi wakiwa katika kambi ya Ifo huko Dadaab, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Kundi hilo linasema shughuli zote ambazo zinaweza kuokoa maisha katika kambi za Daadab zilisitishwa mwezi Octoba baada ya wafanyakazi wake wawili wa msaada kutekwa,

Kundi la Madaktari limesema hali inazidi kuwa mbaya katika makambi makubwa ya wakimbizi nchini Kenya.

Kundi la Madaktari wasio na mipaka –Doctors without Borders, limesema mashirika ya kibinadamu yanataabika kutoa msaada unaotakiwa kwa mahitaji ya kila siku kwa takriban wakimbizi laki nne katika makambi ya Daadab.

Kundi hilo linasema shughuli zote ambazo zinaweza kuokoa maisha katika kambi za Daadab zilisitishwa mwezi Octoba baada ya wafanyakazi wake wawili wa msaada kutekwa, na hali mbaya ya kiusalama kujitokeza. Linasema kuwa huduma zake nyingi bado hazijarejeshwa.

Kundi hilo linasema jumuiya ya kimataifa inashindwa kusaidia kutoa huduma za kawaida kwa wakazi katika makambi na kwa sababu hiyo hali zao zimekuwa mbaya.

Wakimbizi wengi katika kambi za Daadab ni wasomali ambao walitoroka nchini kwao mwaka jana kwa sababu ya njaa na mgogoro wa muda mrefu. Kundi hilo la madaktari wasio na mipaka linasema hali za kiafya kwa wakimbizi hao zinazidi kushuka na kwamba linakadiria mtoto mmoja kati ya 12 katika kambi ana utapiamlo.

XS
SM
MD
LG