Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 04:36

Hali bado ni tete Yemen


Rais wa Yemen Abdrabuh Mansur Hadi.

Mashuhuda wamesema kwamba wanamgambo wa Kishia wamevamia makazi ya rais katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a.

Mapema Jumanne, kikundi cha waasi kinachojulikana kama Houthis kilisema kipo katika mazungumzo kumaliza hali tete baada ya wapiganaji kuzunguka makazi ya Waziri mkuu usiku kucha.

Siku ya Jumamosi, kundi hilo lilimteka kiongozi wa mkuu wa Rais Abed Rabbo Mansour Hadi, wakati serikali ilipokuwa inajaribu kuandika rasimu ya katiba mpya.

Vikosi vya Houthi vinataka usawa mkubwa kwa Washia wachache wa Yemen, walipodhibiti mji mkuu Sana’a, mwezi Septemba, mwaka jana na baadaye kuweka saini makubaliano wakitaka Serikali mpya.

Pamoja na juhudi zote hizo lakini machafuko yameendelea kuikumba nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG