Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 12:52

Haley ni Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa


Balozi Nikki Haley
Balozi Nikki Haley

Baraza la Seneti limempitisha Gavana wa South Carolina, Nikki Haley kuwa balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa ambaye aliteuliwa na Rais Donald Trump.

Maseneta wamemthibitisha kwa urahisi kabisa Gavana wa South Carolina, Nikki Haley katika wadhifa huo, ingawaje hana uzoefu katika masuala ya sera za mambo ya nje za Marekani.

Seneta Bob Corker, mwenyekiti wa warepublikan katika kamati ya mambo ya nje, amesema Haley ni kiongozi mwenye uwezo na “atakuwa mtetezi shupavu” UM kusimamia maslahi ya Marekani.

Kiongozi wa juu wa wademokrat katika kamati hiyo, Seneta Ben Cardin wa Maryland, amesema ametiwa moyo na msimamo wa Haley wa kutokukurupuka katika suala la kupunguza michango ya Marekani ya kifedha katika UM. Marekani imekuwa ikilipa asilimia 22 ya matumizi ya kawaida ya bajeti ya chombo hicho.

Seneta mdemokrat Chris Coons wa Delaware amempinga Haley. Seneta huyo amesema hajashawishika kwamba balozi huyu angeweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

XS
SM
MD
LG