Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema Jumapili kuwa jopo huru limegundua hakuna ushahidi kwamba meli ya Russia ilikusanya silaha nchini Afrika Kusini kwa ajili ya Russia.
Reuben Brigety, balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini alidai mwezi Mei kwamba meli ya Russia ilitia nanga katika kambi ya jeshi la majini ya Simon’s Town karibu na Cape Town ili kupokea shehena ya silaha ambazo zingesafirishwa kwenda Russia.
Hakuna madai yoyote yaliyotolewa kuhusu upokeaji wa silaha kwa Russia ambayo yamethibitishwa ni kweli, Rais Cyril Ramaphosa alisema Jumapili. Hakuna kibali kilichotolewa kwa ajili ya mauzo ya silaha na hakuna silaha zilizosafirishwa nje.
Shutuma hizo ziliibua wasiwasi kuhusu Afrika Kusini kutoegemea upande wowote kwa uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine na huenda likaliweka taifa hilo la Afrika kwa uwezekano wa vikwazo vya Magharibi. Kiongozi wa Afrika Kusini amesema shutuma hizo zilichafua taswira ya nchi hiyo.
Forum