Hakuna haja ya OPEC kuongeza uzalishaji wa mafuta, waziri wa mafuta wa Nigeria Timipre Sylva, alisema Jumanne, hata kama mafuta yanakaribia dola100 kwa pipa, wakati makubaliano muhimu kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani yataongeza mafuta duniani.
Sylva alisema kando ya mkutano wa mawaziri wa nchi zenye kuzalisha gesi nyingi katika mji mkuu wa Qatar Doha kamba “Hatuna haja ya kufanya jambo lolote la kipekee wakati huu kwa sababu ya kwamba, tunatarajia uzalishaji mkubwa,".
Waziri huyo aliongezea kusema kwamba wanatarajia uzalishaji zaidi ikiwa makubaliano ya nyuklia na Iran yatafanikiwa kwasababu kutakuwa na uzalishaji kutoka kwao,.
Mafuta ghafi yaliuzwa chini kidogo ya dola 100 kwa pipa siku ya Jumanne, kiwango chake cha juu zaidi tangu Septemba 2014, kwani uwezekano wa uvamizi wa Russia nchini Ukraine uliongeza hatari ya kupunguka kwa akiba ya mauta.