Kaimu mkurugenzi wa Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, Ahmed Ogwell, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Alhamisi kwamba hakuweza kutoa maelezo zaidi, lakini akasema washirika hao kwa kiasi kikubwa ni taasisi za kimataifa na serikali zisizo za Kiafrika.
Hakuna majadiliano na sekta ya binafsi kwa sababu dozi zote zilizopo tayari zimenunuliwa na nchi nyingine aliongeza.
Vifo vingi zaidi vya Monkey pox vimeripotiwa katika bara la Afrika mwaka huu kuliko popote duniani.
Tangu Mei, karibu nchi 90 zimeripoti kesi zaidi ya 31,000.