Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:48

Kibunga Mathew chaelekea Haiti na Jamaica


Mwanamke ajikinga kutokana na kibunga Mathew kwenye ufukwe wa Les Cayes Haiti mapema Jumatatu.
Mwanamke ajikinga kutokana na kibunga Mathew kwenye ufukwe wa Les Cayes Haiti mapema Jumatatu.

Hali ya tahadhari imetangazwa nchini Jamaica na Haiti, pamoja na baadhi ya maeneo ya Cuba na Bahamas, huku kumbunga kilichopewa jina la Matthew.

Hali ya tahadhari imetangazwa nchini Jamaica na Haiti, pamoja na baadhi ya maeneo ya Cuba na Bahamas, huku kumbunga kilichopewa jina la Matthew, kikiendelea kupita katika pwani ya Caribbean.

Kituo cha kitaifa cha Marekani kuhusu Vibunga, kimesema kuwa Kibunga Mathew, kinaelekea Jamaica na kwamba kitafika eneo la Kusini Magharibi mwa nchi hiyo leo usiku, na Mashariki mwa Cuba kesho Jumanne.

Jamaica na Haiti, zinaendelea kutoa ilani kwa watu walio kwenye maeneo yanayotarajiwa kuathiriwa kuhama na kwenda maeneo salama. Waziri wa mambo ya ndani wa haiti, Francois Anik Joseph, amesema kuwa maafisa wa Serikali wana hofu kubwa kutokana na hali hiyo, na kuongeza kuwa makazi yapatayo 1,300 yameandaliwa, ili kusaidia maelfu ya watu.

Alingoeza kusema kuwa Serikali ingependa wananchi wajue kwamba hali hiyo ni tete na wala si ya kuchukuliwa kwa mzaha.

XS
SM
MD
LG