Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 08:07

Kampeni dhidi ya Kipindupindu yaanza Haiti


Mafuriko yaliosababishwa na Kimbunga Matthew nchini Haiti.
Mafuriko yaliosababishwa na Kimbunga Matthew nchini Haiti.

Haiti imeanza kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya maradhi ya kipindupindu katika baadhi ya sehemu za nchi.

Haiti imeanza kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya maradhi ya kipindupindu katika baadhi ya sehemu za nchi baada kimbunga Matthew kilichotokea hivi karibuni. Kampeni hiyo ilioanza Jumanne inatarajiwa kuwa kubwa zaidi ulimwenguni ikilenga kuwafikia takriban watu 820,000.

Kumekuwa na takriban kesi 3,500 shinazoshukiwa kusababishwa na maradhi yanayoambukizwa kupitia maji machafu baada ya kimbunga hicho cha kiwango cha 4 kilichotokea Haiti mwezi Oktoba na kuuwa watu 546, hali iliopelekea kuenea kwa kipindupindu kutokana na kuharibiwa kwa mabomba ya maji na mkusanyiko mkubwa wa watu waliokoseshwa makazi walioko kwenye kambi za hifadhi.

Kampeni hiyo ni ya kwanza ya aina yake ambapo watu wanapewa chanjo mara moja pekee kinyume na inavyotolewa kwa dosi mbili. Haiti imekuwa ikikabiliana na kipindupindu tangu mwaka wa 2010 baada ya bakteria inayosababisha maradhi hayo kuletwa nchini humo na walinda Amani wa Umoja wa Mataifa. Tangu wakati huo, zaidi ya watu 800,000 wameambukizwa huku wengine 9,000 wakipoteza maisha yao

XS
SM
MD
LG