Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 13:35

Gwiji la muziki akumbukwa


Mchoro unaomuonyesha gwiji la mziki kutoka Nigeria, Fela Kuti
Mchoro unaomuonyesha gwiji la mziki kutoka Nigeria, Fela Kuti

Katika ufunguzi wa maonyesho makubwa mjini Paris ya Philharmonic, mtoto wa gwiji la muziki wa Afrobeat Fela Kuti alizungumzia kuhusu ushujaa wa baba yake wa kutumia muziki kama silaha.
Femi Kuti alisema, baba yake badala ya kukamata bunduki, alitumia muziki, na kuutumia muziki huo kama silaha dhidi ya ukoloni na serikali fisadi za kiafrika. Femi Kuti ambaye ana umri wa miaka 60 sasa, naye pia ni mwana muziki mahiri na mwenye mafanikio makubwa.
Sherehe hizo zilizofanyika kwenye ukumbi wa Paris Philharmonic ni za kumtukuza Fela Kuti kwa kutengeneza mazingira yaliyojaa shamra shamra na msisimko wa harakati za kisiasa kwenye klabu yake ya muziki maarufu iliyokuwa ikijulikana kama The Shrine. Ukumbi huo uliwahi kutembelewa na wanamuziki mashuhuri katika miaka ya 70, kama vile Paul McCartney na Stevie Wonder.
Fela Kuti alifariki kutokana na ugonjwa wa Ukimwi hapo mwaka 1997, lakini kazi zake bado zina nguvu hadi hii leo, mara kwa mara wanamziki wa leo kama vile Flea kutoka kundi la Red Hot Chilli Peppers, au Beyonce na Jay Z ambao walitumia kazi za Fela kama vile kibao chake kiitwacho Zombie, kwenye maonyesho ya Homecoming Live.

Mwanamziki kutoka Nigeria Femi Kuti, mwanawe mwanamziki mashuhuri Femi Kuti kwenye tamasha la Urban Music of Anoumabo mjini Abidjan April 28, 2019
Mwanamziki kutoka Nigeria Femi Kuti, mwanawe mwanamziki mashuhuri Femi Kuti kwenye tamasha la Urban Music of Anoumabo mjini Abidjan April 28, 2019

Femi Kuti mwanawe Fela Kuti, anasema hashangazwi na hayo kwa sababu watu wakubwa kama vile mwanamuziki mahiri Miles Davis aliwahi kumzungumzia Fela Kuti na anasema pia kuwa muziki wa Afrobeat ni mojawapo ya chanzo msingi cha muziki wa Hip Hop, hapo ndipo Afrobeat illipa Hip Hop ladha ya utamu wake.
Fela Kuti naye pia anajihusisha kwenye harakati za kisiasa. Katika maisha yake alikuwa akinyanyaswa na maafisa wa kijeshi kwa kuwa alikuwa akiwakosoa sana juu ya ulaji rushwa na matumizi mabaya ya uongozi.
Hapo mwaka 1977 baada ya kukata kushiriki kwenye tamasha la muziki la kiserikali, aliamua kuandaa shughuli nyingine wakati huohuo ambapo lilikuwa na hamasa na umaarufu mkubwa na lilihudhuriwa na waimbaji mashuhuri wakiamtaifa akiwemo Stevie Wonder.
Wanajeshi walijibu tamasha lake kwa kuchoma nyumba ya Femi na kumsukuma mamake kutoka kwenye dirisha la ghorofa ya kwanza, na kusababisha majeraha yaliyopelekea kifo chake mwaka mmoja baadae.
Femi Kuti anasema baba yake, Fela kuti, alikuwa sauti ya wasiokuwa na sauti, mpinzani jasiri aliyepambana na madikteta sugu wa kijeshi, na hali hiyo ilimgharimu sana Fela Kuti.
Lakini hatimaye, ubora wa muziki wake ndio uliomfanya kuwa maarufu sana akibuni mchanganyiko wa muziki baina ya free jazz, soul, funk na Yoruba.
Paul McCartney ni mmoja wa wanamuziki waliowahi kuzuru ukumbi wa klabu ya Fela, The Shrine, ambako pia alirekodi album yake ya “Band on the Run” kwenye ukumbi huo.
Femi Kuti anasema baba yake Fela, alikuja na muziki huu maarufu sana wa Afrobeat ambao uliwanasa wote waliousikia.
Kutumia muziki kama silaha ya kisiasa na ujumbe ulipata mtizzamo wa dunia na hususan taifa la Ufaransa pengine kwa sababu ya uhusiano kwa uasi wao wenyewe.

XS
SM
MD
LG