Msemaji wa Guterres amesema mkuu huyo wa Umoja wa mataifa atazuru baadaye siku ya Alhamisi mjini Kyiv kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, kwa sababu Guteress anaamini kuna “ fursa halisi” ya kupiga hatua.
Akiwa njiani kuelekea Moscow, Guterres alikutana Jumatatu mjini Ankara na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye alijaribu bila mafanikio kuwapatanisha, na kumaliza vita kati ya majirani hao wawili wanaoshirikiana bahari na Uturuki.
Guterres ametoa wito mara kadhaa wa kusitisha mapigano kwa ajili ya shughuli za kibinadamu au kusitisha mapigano kwa muda, lakini bila mafanikio.