Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameutaka ulimwengu leo Jumatatu “kuacha kuchukizwa” na mabadiliko ya hali ya hewa wakati alipotembelea maeneo ya Himalaya yanayokabiliwa na hali ya kuyeyuka theluji kwa kasi ili kushuhudia athari mbaya za hali hiyo.
“Mapaa ya dunia yanaingia”, alisema Guterres katika ziara yake katika eneo la Everest katika milima ya Nepal akiongeza kuwa nchi hiyo imepoteza karibu theluthi moja ya barafu yake katika kipindi cha miongo mitatu.
Theluji za Nepal ziliyeyuka kwa asilimia 65 kwa kasi katika muongo uliopita kuliko ile ya awali, alisema Guterres, ambaye yuko katika ziara ya siku nne nchini Nepal. Theluji katika eneo pana la Himalaya na Hindu Kush ni chanzo muhimu cha maji kwa takribani watu milioni 240 katika maeneo ya milima, na pia kwa watu wengine bilioni 1.65 katika mabonde ya mito huko Asia Kusini, na Asia Kusini Mashariki.
Forum