Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 09:06

Mashambulio ya bunduki yazuka Abidjan


Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa huko Abidjan, Ivory Coast
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa huko Abidjan, Ivory Coast

Milio ya risasi imezuka katika mji mkuu wa kibiashara huko Ivory Coast na kuwauwa watu wawili wakati mapambano ya kuwania madaraka ya kisiasa yakiendelea katika taifa hilo la Afrika magharibi.

Mashahidi wanasema ghasia zilizuka leo Jumanne katika mji wa Abidjan kati ya majeshi ya usalama yanayomtii rais aliyeko madarakani Laurent Gbabgbo na wafuasi wa Alassane Ouattara, mshindi anayetambulika kimataifa kufuatia uchaguzi wa Rais wa mwezi Novemba.

Mapigano yalitokea katika eneo linalomuunga mkono Ouattara liitwalo Abobo.
Shirika la habari la Associated Press linaripoti walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliondoka kutoka eneo hilo baada ya majeshi ya usalama kufyatua risasi.

Bwana Ouattara bado anaishi katika hoteli ya Abidjan iliyolindwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa. Rais aliyeko madarakani Laurent Gbagbo ambaye anaendelea kudhibiti jeshi anakataa kuachia madaraka licha ya shinikizo la kimataifa kumtaka afanye hivyo.

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga anatarajiwa kurudi Ivory Coast wiki hii katika juhudi za mazungumzo ya kumaliza ghasia zilizopo. Bwana Odinga anahudumu kama mpatanishi wa nchi hiyo katika Umoja wa Afrika.

Katika hatua nyingine shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema wananachi wa Ivory Coast 25,000 wamekimbilia Liberia kwa sababu wanakhofia mgogoro wa kisiasa utapelekea ghasia kusambaa.

XS
SM
MD
LG