Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 11:24

Guinea: Waziri wa zamani afariki gerezani


Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Guinea Kanali Mamadi Doumbouya, picha ya Reuters.

Waziri wa zamani ambaye alifungwa jela na utawala wa kijeshi nchini Guinea alifariki gerezani, kaka yake ametangaza.

Lounceny Camara, mwenye umri wa miaka 62, ni miongoni mwa mawaziri wa zamani na maafisa waandamamizi walioshtumiwa ubadhirifu wa pesa za umma na kufungwa jela baada ya jeshi kumuondoa madarakani rais wa zamani Alpha Conde mwaka uliopita.

Camara alipatwa na kiharusi Ijumaa na alifariki hospitalini jioni iliyofuata, kaka yake ameiambia AFP.

Familia yake ilikata rufaa mahakamani bila mafanikio ili Camara aruhusiwe kusafiri nje ya nchi kupata matibabu, ameongeza.

Camara alikuwa tayari amelazwa hospitali mara moja kabla ya kufungwa kwake, mapema mwezi Mei baada ya kufungwa jela.

Waziri wa sheria Charles Alphonse Wright amesema katika taarifa iliyosomwa na vyombo vya habari vya nchini humo kwamba Camara alipata matibabu aliyohitaji katika hospitali ya chuo kikuu cha Conakry.

Camara alikuwa amefunguliwa mashtaka ya ubadhirifu wa pesa za umma na mashtaka mengine yanayohusiana na ufisadi.

Alikuwa mwanachama mkuu wa chama cha Alpha Conde, Rally for the Guinean People (RPG).

Shirika linalotetea haki za binadamu Amnesty International, ambalo limekuwa likikosoa vikali hali ya haki za binadamu nchini Guinea, lilisema mwezi Februari mwaka wa 2021 kwamba magereza nchini humo yanajulikana kwa kudhulumu haki za wafungwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG