Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:55

Antonio Guterres ateuliwa kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa


Antonio Guterres.
Antonio Guterres.

Waziri mkuu wa zamani wa Ureno Guterres ameteuliwa kuwania nafasi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na anatarajiwa kuidhinishwa katika siku chache zijazo.

Kufuatia upigaji kura usio rasmi uliofanyika Jumatano kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,mwanasiasa huyo mkongwe na mwanadiplomasia wa siku nyingi alipata kura 13 za kumuunga mkono,na kura mbili ambazo hazikueleza msimamo wa wanachama hao wawili.

Mjumbe wa Russia kwenye Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin alitoa tangazo hilo kama Rais wa Baraza hilo. Alisema kuwa wamepata kiongozi anayependelewa na wengi na akiongozea kuwa kura rasmi itafanyika Alhamisi.

XS
SM
MD
LG