Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 01:06

Serikali ya Marekani yafungwa


Bunge la Marekani
Bunge la Marekani

Serikali ya Marekani imefunga baadhi ya shughuli zake kuanzia mapema Jumamosi baada ya baraza la Seneti kushindwa kupitisha mswaada wa matumizi ya serikali. Matumizi ya serikali yalimalizika saa sita usiku Ijumaa kwa saa za Washington, na hivyo kusimamishwa shughuli zisizo za lazima.

Baadhi ya maseneta Warepublican walijunga na sehemu kubwa ya Wademokrat kupinga mswaada huo, ambao ulihitaji kura 60 kupita katika baraza hilo lenye wajumbe 100.

Baraza la Seneti liliahirisha kikao chake mpaka saa sita mchana Jumamosi ambapo maseneta wanatazamiwa kuendelea na majadiliano ya kupitishwa mswaada wa matumizi ya serikali.

Kwa kushindwa kufikia makubaliano Ijumaa maseneta wa bunge la Marekani sasa watalazimika kuwa na majadiliano ya dharura ndani na nje ya bunge kupata makubaliano ya mwisho mwisho ambayo yatapitisha matumizi ya serikali.

Mara ya mwisho serikali ya Marekani ilifunga shughuli zake kwa siku 16 baada ya kukosa fedha za matumizi mwaka 2013 katika utawala wa Rais Barack Obama.

XS
SM
MD
LG