Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 22:56

Goodluck Jonathan Rais Mpya Nigeria


Rais mpya wa Nigeria (kulia) Goodluck Jonathan akimpongeza waziri wake mpya wa Fedha Olusegun Aganga
Rais mpya wa Nigeria (kulia) Goodluck Jonathan akimpongeza waziri wake mpya wa Fedha Olusegun Aganga

Goodluck Jonathan ni rais mpya wa Nigeria.

Goodluck Jonathan ni rais mpya wa Nigeria. Aliapishwa Alhamisi saa chache baada ya kifo cha rais Umaru Yar’Adua.

Ilikuwa ni hafla ya ukimya kwa rais mpya ambaye amekuwa akiendesha nchi hiyo kwa miezi kadhaa kwa sababu ya kutokuwepo kwa muda mrefu kwa hayati rais aliyeugua kwa muda mrefu.

“Mimi Goodluck Ebele Jonathan naapa kwamba nitakuwa mwaminifu na kuwa mzalendo wa kweli kwa Jamhuri ya Nigeria, nitafanya kazi yangu kwa uwezo wangu wote, kwa uaminifu kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Nigeria.”

Rais Jonathan aliahidi kufuata sheria zote na kutawala kwa matakwa ya uhuru, uaminifu, umoja , ubora na ustawi wa Nigeria.

“Sitaruhusu matakwa binafsi kuingilia ufanyaji kazi wangu au maamuzi ya kikazi” alisema Bw. Jonathan.

XS
SM
MD
LG