Ghasia zimeanza tena kaskazini mwa Nigeria Jumatatu wakati watu wenye silaha wanaoaminika kuwa wanachama wa kundi la kiislam la Boko Haram kushambulia kituo cha Polisi huko Kano.
Mkuu wa Polisi wa eneo hilo Ibrahim Idris alithibitisha shambulio hilo lakini hakutoa taarifa zaidi.
Shambulio jingine lilitokea Jumatatu huko Maiduguri mashariki mwa Kano, ambapo soko lilishambuliwa. Hakukuwa na ripoti za vifo au majeruhi katika mashambulizi hayo mawili.