Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 02:20

Ghasia za kidini zinazuka tena Misri


Wamisri wa dhehebu la Coptic wakiandamana Jumapili mjini Cairo kulaani ghasia za kidini za siku mbili kati ya waislamu na wakristo.katika kitongoji cha Imbaba Cairo., May 8, 2011.

Maelfu ya wakristo wa dhehebu la Coptic wanaolalamika dhidi ya kuzuka upya mauwaji na ghasia za kidini wanataka kuondolewa kwa mkuu wa majeshi Marshali Mohamed Hussein Tantawi na wameapa kutondoka mbele ya jingo la televisheni ya taifa mjini Cairo.

Waandamanaji walojitokeza Jumapili usiku mjini Cairo walimtaka Marshali Tantawi ajiuzulu na wale walohusika na kutia moto kanisa mbili za dhehbu la Coptic kufikishwa mahakamani. Waandamanaji wanataka uchochezi wa ghasi za kidini kuwa ni uhalifu nchini Misri.

Vyombo vya habari vya Misri vinaripoti kwamba watu 12 wameuwawa na zaidi ya 220 kujeruhiwa wakati wa mapigano ya kidini ya siku mbili yaliyoanza Jumamosi usiku katika kitongoji cha Imbaba, cha watu maskini mjini Cairo.

Mashahidi wanasema kundi la takriba watu 500, waislamu wenye siasa kali wa dhehabu la Salafist walikusanyika nje ya kanisa moja la dhehbu la Coptic kujibu uvumi kwamba mwanamke mmoja wa kikristo alikuwa anashikiliwa ndani akizuiliwa kubadili dini na kuwa muislamu.

Ripoti nyengine zinasema watu nje waliamini mwanamke alikuwa ameshabadili dini na alikuwa anazuiliwa mumowa mwanamume muislamu. Amri ya kutotoka nje imetangazwa katikja kitongoji hicho.

Viongozi wa kisaisa wa Misri wameahidi kuchukua hatua thabiti kukabiliana na ghasia hizo ikiwa ni pamoja ulinzi mkali wa nyumba zakuabudu na marufuku mpya nje ya kanisa na misikiti.

Viongozi wa kidini wametowa wito wa kuitishwa mkutano wa dharura kujadili na kudhibiti ghasia za kideni nchini humo.

XS
SM
MD
LG