Shirika la habari la Ufaransa-AFP linaripoti kwamba watu wawili wameuwawa na zaidi ya 40 kukamatwa katika ghasia za kabla ya uchaguzi katika vitongoji vya mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria, kwa mujibu wa polisi.
Msemaji wa polisi Noxolo Kweza alisema watu wawili waliuwawa usiku wa Jumanne baada ya kutokea wizi kwenye maduka katika mji wa Mamelodi kufuatia maandamano ya ndani ya chama tawala cha African National Congress-ANC yanayohusiana na uchaguzi ujao wa serekali za mitaa.
Ghasia zilizotokana na mabishano yaliyotokea Jumatatu jioni dhidi ya chaguo la mgombea wa umeya wa chama tawala cha ANC mjini Pretoria katika uchaguzi wa Agosti 3.