Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 11:16

Ghasia za zuka tena Arusha


Wafuasi wa chama cha CHADEMA wakiwa kwenye uwanja wa Soweto Arusha
Wafuasi wa chama cha CHADEMA wakiwa kwenye uwanja wa Soweto Arusha
Polisi wa kukabiliana na ghasia wamevamia uwanja wa Soweto jijini Arusha siku ya Jumanne kutawanya wafuasi wa chama cha upinzani cha CHADEMA, waliokuwa wanataka kukusanyika ili kuaga miili ya wenzao waliofariki kufuatia ghasia zilizotokea Jumapili.

Mapema siku ya Jumanne kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Leberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea kwenye uwanja huo kufuatia shambulio la bomu la siku ya Jumapili haitokuwa jambo la busara kuweka mkusanyiko wa watu katika eneo hilo.

Aliongeza kusema kufanya hivyo kutaweza kuharibu upelelezi, na hivyo kikosi cha polisi kimewataka wakuu wa chama cha CHADEMA kuwaeleza wafuasi wao waelekee mahala pengine watakapoweza kuendelea na shughuli zao.

Kufuatana na mwandishi wa Sauti ya Amerika huko Arusha, Viongozi wa chama hicho walifika kwenye uwanja huo na kuwaeleza wafuasi wao kuelekea hadi hospitali ambako miili ya waliouliwa imewekwa. Lakini anasema hata kabla ya kumaliza maelezo yao polisi waliwavamia na kufyatua mabomu ya kutoa machozi kutawanya watu.

Tangu kutokea shambulio la bomu siku ya Jumapili huko Arusha chama tawala nchini Tanzania cha CCM na kile cha upinzani cha CHADEMA vimekuwa vikilaumiana kwa ghasia hizo.

Akizungumza na Sauti ya Amerika katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, amesema, '"sisi Chama cha Mapinduzi, tunaamini tukio hili lilipangwa na lilipangwa na CHADEMA wenyewe."

Mahojiano na Nape Nnuaye - 4:01
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:01 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anaedai yeye na mkuu wa chama Freeman Mbowe, ndio waliokuwa wamelengwa kuuliwa katika shambulio hilo."Ni uwenda wazimu kwamba unaweza ukajirushia bomu halafu lije likuuwe. Unaona kiasi gani chama tawala kimekosa fikra na busara ya kutawala nchi."

Chama cha CHADEMA kilipanga kuaga miili ya watu wanne waliouliwa katika ghasia za Jumapili na kutangaza nani wanaoamini aliyefanya shambulio hilo.
XS
SM
MD
LG