Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 23:46

Ghadafi asema kugawanyika kwa Sudan ni hatari


Rais wa Libya , Muammar Gadhafi
Rais wa Libya , Muammar Gadhafi

Viongozi wa kiarabu na wa kiafrika wana kongamano katika mji wa mapumziko wa Sirte nchini Libya linalokutanisha watu wenye asili ya kiafrika na kiarabu,

Ghadafi asema kugawanyika kwa Sudan ni hatari

Viongozi wa kiarabu na wa kiafrika wana kongamano katika mji wa mapumziko wa Sirte nchini Libya linalokutanisha watu wenye asili ya kiafrika na kiarabu, kuzungumzia ushirikaino zaidi katika nyanja mbali mbali.

Kiongozi wa Libya Moammar Ghadafi ambaye aliongoza mkutano huo, alionya dhidi ya kugawanyika kwa Sudan, kufuatia kura ya maoni iliyopangwa kufanyika hapo mwezi Januari.

Ghadafi alisisitiza kuwa mzozo wowote utakaotokea huko Sudan, utaenea kutoka Afrika hadi nchi nyingine za kiarabu na itakuwa vigumu kuzuia migawanyiko katika nchi za kiarabu.

Aidha kiongozi huyo wa Libya alidai kuwa kuvunjika kwa Sudan katika pande mbili za Kaskazini na Kusini huenda kukatishia bara zima la Afrika.

XS
SM
MD
LG