Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 15:12

George H.W. Bush ahamishiwa ICU


George H.W. Bush akiwa na mkewe Barbara na wajukuu zao, Barbara(Kushoto) na Jenna
Rais wa zamani wa Marekani, George H.W.Bush amelezwa kwenye chumba cha wagonjwa mahtuti -ICU katika hospitali moja huko Houston katika jimbo la Texas nchini Marekani.
Kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 88 alilazwa hospitalini mwezi uliopita akiwa na tatizo la kupumua.

Msemaji wake anasema bwana Bush alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi Jumapili baada ya kupata homa kali. Aidha msemaji huyo anasema rais huyo wa zamani anaendelea kuangaliwa kwa karibu na kwamba madaktari wana matumaini kuhusu matibabu yake.

Mkewe Barbara Bush na mtoto wake mmoja wa kiume pamoja na mjukuu wa kiume walisheherekea sikukuu ya Krismas hospitalini hapo na bwana Bush.
XS
SM
MD
LG