Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 04:43

Mkimbiaji Gebreselassie wa Ethiopia astaafu


Haile Gebreselassie, wa pili kushoto, akiwa katika mbio ndefu za New York
Haile Gebreselassie, wa pili kushoto, akiwa katika mbio ndefu za New York

Mwanariadha bingwa katika mbio ndefu - marathon - Haile Gebreselassie wa Ethiopia ametangaza kustaafu katika mchezo huo Ijumaa baada ya kuiwakilisha Ethiopia katika mashindano kadha kwa miaka 25 iliyopita.

Gebreselassie, mwenye umri wa miaka 42, aligusia kuwa anakaribia kustaafu mwezi Mei mwaka huu wakatika wa mashindano ya Great Manchester Run, shindano maarufu na kubwa barani Ulaya ambalo linafanyika Manchester, Uingereza.

Gebreselassie anajulikana kwa kuweka rekodi 27 za dunia, ana medali za dhahabu za Olimpiki mbili na alishinda ubingwa wa dunia mara nane katika mbio hizo za marathon.

Akizungumza na VOA kutokea Addis Ababa, Gebreselassie alisema anashukuru sana kupata fursa ya kushiriki katika mashindano mengi, lakini ushindi anaoukumbuka sana ni ule wa katika mita 10,000 wakati wa michezo ya Olimpiki mjini Sydney, Australia, mwaka 2000.

Mwanariadha huyo ambaye alikuwa na ushindani mkubwa na wanariadha wa kutoka Kenya anasifu familia yake na marafiki ambao walimsaidia katika matayarisho na kumwunga mkono wakati wote akiwa katika mashindano.

XS
SM
MD
LG