Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 05:58

Gavana wa New York Andrew Cuomo ajiuzulu


Andrew Cuomo gavana wa New York ametangaza kujiuzulu baada ya kukumbwa na kashfa za manyanyaso ya kijinsia
Andrew Cuomo gavana wa New York ametangaza kujiuzulu baada ya kukumbwa na kashfa za manyanyaso ya kijinsia

Gavana Andrew Cuomo wa New York ametangaza kujiuzulu kwa sababu ya mfululizo wa madai ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi yake.

Gavana Andrew Cuomo wa New York ametangaza kujiuzulu Jumanne kwa sababu ya mfululizo wa madai ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi yake ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kusifiwa sana kitaifa kwa maelezo yake ya kina ya kila siku na uongozi wakati wa siku za giza za maambukizi ya COVID-19.

Uamuzi wa gavana huyo aliyeongoza kwa mihula mitatu ulitangazwa wakati kasi iliongezeka katika Bunge la jiji hilo kumwondoa madarakani kwa kumfungulia mashitaka. Uamuzi huo ulikuja baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa jiji la New York kutoa matokeo ya uchunguzi uliomkuta na hatia ya kunyanyasa kijinsia takriban wanawake 11.

Wachunguzi walisema aliwapiga busu wanawake bila ridhaa yao, aliwashika matiti yao au makalio au vinginevyo aliwagusa vibaya; alitoa maneno ya kashfa dhidi ya sura zao na maisha yao ya kimapenzi na kusababisha mazingira ya kazi yaliyojaa hofu na vitisho.

Naibu Gavana Kathy Hochul, Mdemocrat mwenye umri wa miaka 62 na mbunge wa zamani wa eneo la Buffalo, atakuwa gavana wa 57 wa jimbo hilo na mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.

XS
SM
MD
LG