Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 22:22

Garland amtetea mwendesha mashtaka maalum anayeshughulikia kesi ya Trump


Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Merrick Garland. April 14, 2023.

Trump amekuwa akimkosoa Smith mara kwa mara katika ujumbe wake wa mitandao ya kijamii. Amemuita mwendesha mashtaka huyo kuwa mhalifu na mzushi maneno ambayo pia aliyatoa Jumanne wakati Trump alipokana hana hatia kwa mashtaka 37 yaliyofunguliwa na Jack Smith

Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland siku ya Jumatano alimtetea Jack Smith, mwendesha mashtaka mzoefu ambaye alimteua kama wakili maalum wa kujitegemea kushughulikia uchunguzi wa uhalifu kwa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

Trump amekuwa akimkosoa Smith mara kwa mara katika ujumbe wake wa mitandao ya kijamii. Amemuita mwendesha mashtaka huyo kuwa mhalifu na mzushi, maneno ambayo pia aliyatoa Jumanne, wakati Trump alipokana kuwa hana hatia katika mahakama ya Marekani mjini Miami kwenye jimbo la Florida, kwa mashtaka 37 yaliyofunguliwa na Smith.

Waraka huo ulimshutumu Trump, kwa makusudi kuhifadhi nyaraka 31 za usalama wa taifa, na kula njama ya kuzificha wakati mamlaka za serikali kuu zilipomtaka azikabidhi.

Garland alisema “Kama nilivyosema wakati nilipomteua Smith, nilifanya hivyo kwa sababu inasisitiza nia ya dhati ya Idara ya Sheria, kwa vyote, uhuru na uwajibikaji", Garland, afisa wa cheo cha juu wa utekelezaji wa sheria Marekani aliwaambia waandishi wa habari katika Idara ya Sheria anayoongoza.

Forum

XS
SM
MD
LG