Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2020 Local time: 14:35

Mlipuko waua 11 Uturuki


Gavana wa jiji la Istanbul mapema leo amethibitisha kuwa watu 11 ikujumuisha maafisa wa polisi 7 wameuwawa na 36 kujeruhiwa katika mlipuko katikati ya Instanbul nyakati za asubuhi watu wakielekea makazini.

Gari lililokuwa na milipuko lililipuka wakati likiipita basi waliokuwamo kikosi cha polisi cha kutuliza ghasia.

Magari kadhaa ya wagonjwa yalipelekwa katika wilaya ya kati ya Vezneciler, karibu na Chuo Kikuu cha Istanbul na kituo maarufu cha utalii cha “Bayezit Square.”

Hakuna kundi ambalo limetangaza kuhusika na shambulizi hilo, japo Islamic State siku za karibuni imefanya mashambulizi nchini Uturuki.

Chama cha Kikurdi cha PKK pia kimekuwa kikuwalenga polisi na jeshi la Uturuki toka mwezi Julai mwaka jana katika mapambano yao ya kutaka kujitenga kwa eneo la Kusini Mashariki.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG