Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 09:35

Rais wa Gambia aonyesha mfano Afrika kukubali matokeo

wafuasi wa rais mteule wa Gambia ,Adama Barrow wakisherehekea ushindi wa mgombea wao.
wafuasi wa rais mteule wa Gambia ,Adama Barrow wakisherehekea ushindi wa mgombea wao.

Katika hotuba yake ya kukubali matokeo iliyotangazwa kwenye televisheni Yahya Jammeh alimpongeza mpinzani wake Adama Barrow kwa ushindi alioupata na kusema kuwa uchaguzi ulikuwa wazi bila kuibwa.

Rais wa Gambia kwa takriban miaka 22 amekubali kushindwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika wiki hii, hivyo kutekeleza ahadi yake ya kung’atuka madarakani endapo angeshindwa uchaguzi.

Katika hotuba yake ya kukubali matokeo iliyotangazwa kwenye televisheni Yahya Jammeh alimpongeza mpinzani wake Adama Barrow kwa ushindi alioupata na kusema kuwa uchaguzi ulikuwa wazi bila kuibwa.

Jammeh pia alisema kwamba “Mola anamwambia muda wake umekwisha” na atahamia katika shamba lake baada ya kuondoka madarakani mwezi Januari.

Tume huru ya uchaguzi nchini Gambia ilitangaza Ijumaa kwamba Barrow ameshinda kwa kura 263,000 ambazo ni sawa na asilimia 45 wakati Jammeh alipata kura 212,000 ambazo ni sawa na asilimia 36. Mgombea wa tatu Mamam Kandeh alikuwa nyuma zaidi.

Barrow mwenye umri wa miaka 51 aliwakilisha ushirikiano wa vyama vya upinzani vilivyotoa changamoto dhidi ya Jammeh katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi iliyopita.

Jameh aliongoza taifa hilo dogo la afrika magharibi tangu alipoingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1994. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakimshutumu Jammeh kwa kuwakamata wapinzani wa kisiasa na waandishi wa habari na mara nyingine kuamuru wauwawe.

XS
SM
MD
LG