Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:36

Gambia haipaswi kuaminika


Rais wa Gambia, Yahya Jammeh
Rais wa Gambia, Yahya Jammeh

Hatua za Serikali ya Gambia kufuatia jaribio la mapinduzi Desemba 30, mwaka jana, zimekuwa si zakuaminika kwa mujibu wa makundi vya kutetea haki za binadamu ambayo yanasema darzaeni ya raia na wanajeshi wameshikiliwa.

Suala hili limechukua mrengo wa kimataifa hasa kwa kukamatwa kwa washukiwa wengine wa jaribio hilo nchini Senegal na Marekani.

Kauli ya makundi hayo inafuatia habari kwamba serikali ya Senegal, inatafakari juu ya kumsafirisha au kumuondoa nchini humo kiongozi wa upinzabni wa Gambia aliyetowa wito kwa wananchi kujitokeza na kumpindua kiongozi wa muda mrefu Yahya Jammeh, wakati wa kutangazwa kwa jaribio la mapinduzi.

Rais Jammeh alichukua hatua za haraka na kuwauwa viongozi wa jaribio hilo na inaripotiwa kwamba maafisa wa usalama wamewakamata baadhi ya watu wa karibu na viongozi wa jaribio hilo.

Hali ya usalama imeendelea kuimnarishwa nchini humo wiki moja baada ya washambuliaji wenye silaha kujaribu kuipindua serikari.

Maafisa wa usalama wanaendelea kuwakaguwa watu kwenye mipaka na vituo katika barabara kuu yakuelekea mji mkuu.

Wengi waliodhaniwa kuhusika inaaminika wametorokea nje ya nchini.

Makundi ya kutetea haki za binadamu ikiwemo Amnesty International, yameonya dhidi ya kurudishwa kwa watuhumiwa huko Gambia.

Mkurugeni wake huko Senegal anasema hiyo itakuwa ni kashfa kubwa kwa kumrudisha mtu yeyote.

Iliripotiwa awali kwamba Guinea Bissau, imewakamata baadhi ya raia wa Gambia, lakini serikali ilikanujsha jambo hilo.

XS
SM
MD
LG